Karbala yashuhudia igizo lililo sababisha vilio kwa wahudhuriaji kutokana na yaliyojiri mwezi kumi Muharam

Maoni katika picha
Kwa kushirikiana na kitengo cha Mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, chama cha Zaharaa (a.s) kutoka mkoa wa Diwaniyya kwa mwaka wa tatu mfululizo, asubuhi ya Alkhamisi (12 Muharam 1441h) sawa na (12 Septemba 2019m) wameshuhudia igizo lililo fanywa katika jangwa lililopo barabara ya Karbala/Najafu, lililo onyesha mauwaji yaliyo tokea mwezi kumi Muharam na yaliyo endelea baada ya mauwaji hayo, maonyesho ya igozo hilo yamehudhuriwa na watu wengi kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, ukiwemo ujumbe maalum wa Atabatu Abbasiyya tukufu uliokua na mchango mkubwa katika maandalizi ya igizo hilo.

Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kazi ya uigizaji ni moja ya aina ya maombolezo ya Husseiniyya, humfanya mtu ahisi yaliyo tokea kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), chama cha Zaharaa kimeandaa igizo zuri linalo onyesha yaliyo jiri katika uwanja wa Karbala”.

Naye bwana Haadi Atwishani kiongozi wa chama za Zaharaa (a.s) ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kwa mwaka wa tatu mfululizo chama cha Zaharaa tumekua tukiigiza yaliyo jiri katika uwanja wa Karbala, ikiwa ni pamoja na yaliyo tokea kwa Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake mwezi kumi Muhara mwaka wa (61h), tumekua tukiandaa igizo hili kwa zaidi ya miezi sita, baada ya kukubaliana na uongozi wa mkoa wa Karbala, pamoja na kitengo cha Mawakibu Husseiniyya cha Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kuanzia kuandaa mahema na kufanya mazowezi”.

Akaongeza kua: “Jumla ya watu wanao wakilisha jeshi la Umawiyya ni (1200), na idadi ya watu wanao wakilisha watu wa Imamu Hussein (a.s) ni (72) pamoja na wanawake na watoto, maneno yanayo zungumzwa katika igizo hili yamefanyiwa uhakiki na wanachuoni wa Najafu”.

Kumbuka kua fani ya uigizaji imepata maendeleo makubwa katika miaka ya hivi karibuni, kwani hutumika watu waliosomea mambo ya uigizaji ili kuonyesha mazingira halisi ya tukio la Twafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: