Watu wa Karbala kizazi kwa kizazi wamezowea kufanya maombolezo na kutoa huduma kwa mazuwaru katika kumi la kwanza la mwezi wa Muharam, hawaja katazwa kushiriki watu wengine lakini toka zamani imekua ni desturi yao, unapo karibia mwezi wa Muharam wanafanya maandalizi ya kutoa huduma kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), maukibu za watu wa Karbala ni sawa na mawakibu zingine za Husseiniyya, zimegawanyika sehemu mbili: maukibu za kuomboleza na maukibu za kutoa huduma.
Kuanzia siku ya kwanza ya Muharam watoto kwa wazee wanawake kwa wanaume hufanya kazi ya kuwahudumia mazuwaru, kwa kuwapa chakula, vinywaji, sehemu za kulala pamoja na huduma zingine hadi mwezi kumi Muharam, na kuna maukibu ambazo huendelea kutoa huduma hadi siku ya kumbukumbu ya mazishi ya Imamu Hussein (a.s) mwezi kumi na tatu Muharam, na zingine huendelea kubaki hadi baada ya siku hiyo.
Mawakibu na vikundi vya Husseiniyya hufanya kila wawezalo katika kuwahudumia mazuwaru, utawakuta wamevaa nguo nyeusi wakiandaa vyakula vya aina mbalimbali kwa ajili ya kugawa bure, ili kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu kwa utukufu wa Ahlulbait (a.s). mazingira yao yakisema: Kila tunacho miliki ni kwa utukufu wa Abu Abdilla Hussein (a.s) yeye ndio utukufu wetu duniani na muombezi wetu akhera.