Watumishi wa Abulfadhil Abbasi wanaomboleza siku ya saba tangu kuuwawa kwa Imamu Hussein (a.s) pamoja na watu waliofariki kwa ajili yake katika matembezi ya Towariji

Maoni katika picha
Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kama kawaida yao katika kila msimu wa Ashura hufanya kumbukumbu ya siku ya saba tangu kuuwawa kwa Imamu Hussein (a.s) na kuelekeza rambirambi zao kwa Imamu wa zama Hujjat bun Hassan (a.f), huku mazingira yao yakionyesha kua: (Ikiwa hakuhudhuria yeyote katika kaburi lako siku ya saba ya kifo chako sisi watumishi wako tumesimama mbele ya kaburi lako na kuomboleza”, maombolezo haya yanafanyika sambamba na maombolezo ya watu walio fariki katika matembezi ya Towariji.

Maombolezo yalianza baada ya Adhuhuri ya mwezi (17 Muharam 1441h) sawa na (17 Septemba 2019) katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuelekea katika malalo ya bwana wa mashahidi (a.s) na kutuma rambirambi kwa Imamu wa zama (a.f) wakiwa wamebeba mishumaa kama ishara ya kuomboleza msiba wa Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake.

Matembezi hayo yamepambwa na kaswida mbalimbali za uombolezaji zinazo onyesha mapenzi na utiifu wa watumishi wa Ataba mbili tukufu kwa Ahlulbait (a.s) na kushikamana na mwenendo aliobakiza kupitia damu yake takatifu, ambao ni muendelezo wa mafundisho ya babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), kisha wakafanya majlis ndani ya haram tukufu sambamba na kuwakumbuka mashahidi wa matembezi ta Towariji ya mwezi kumi Muharam.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: