Mafunzo hayo yanafanyika ndani ya ukumbi wa Qassim (a.s) katika Atabatu Abbasiyya na kusimamiwa na walimu mahiri walio peana majukumu ndani ya siku zote kumi, kila siku itakua na mada mbili au tatu, siku ya kwanza ilikua na mada zisemazo:
- - Uandaaji wa andiko: imewasilishwa na Ustadh Swabaah Rahimah
- - Utambulisho wa hafla: umefanywa na Ustadh mwanahabari maarufu Haidari Salami.
- - Usanifu: imewasilishwa na ustadh Nurdini Rahmani kwa kushirikiana na Ustadh Ali Auni.
Ratiba hiyo itaendelea hadi mwisho chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ukiwa ni muendelezo wa kuwajengea uwezo watumishi kulingana na fani zao, ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao, semina hii ni ya kwanza kufanywa na idara ya watoto na makuzi.