Ujembe wa wanasekula umetembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu na wameisifu kua ni fahari kwa taifa

Maoni katika picha
Miongoni mwa sehemu za mapumziko yaliyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa walimu wa sekula waliokuja katika semina ya Quráni Aljuud, ilikua ni kutembelea miradi ya Ataba tukufu na kuangalia maendeleo ya miradi hiyo, aidha kutambua huduma zinazo tolewa kwa raia wa Iraq.

Wametembelea hospitali ya rufaa Alkafeel, kiwanda cha uchapishaji wa vitabu Alkafeel, shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa ya viwanda na kilimo Aljuud na shirika la Nurul-Kafeel la kuzalisha bidhaa za vyakula.

Mmoja wa walimu aliyekuwepo katika matembezi hayo Dokta Saadi Muhammad Hilali kutoka chuo kikuu cha kiislamu tawi la Baabil amesema: “Tumeshangwazwa na miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa hakika imedhulumiwa na vyombo vya habari, tunavilaumu vyombo hivyo kwa kutotangaza miradi hii muhimu ambayo ni fahari kwa taifa, kutokana na huduma kubwa wanayo pata raia wa Iraq kwenye sekta mbalimbali, sambamba na kuajiri maelfu ya wananchi wa Iraq”.

Akaongeza kua: “Tunamshukuru Mwenyezi Mungu Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na wizara ya malezi na elimu, imefanikiwa kumaliza tatizo la kuchapisha vitabu na madaftari ndani ya Iraq badala ua kuchapishwa nje ya nchi, hili ni jambo la kujivunia”.

Fahamu kua semina ya Quráni Aljuud inayo simamiwa na Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya inafanyika kwa muda wa siku (7) ndani ya jengo la Imamu Haadi (a.s) ikiwa na washiriki zaidi ya (50) ambao ni walimu kutoka vyuo vikuu (13) vya Iraq, nayo ni miongoni mwa miradi inayo kusudia kufundisha maadili ya Quráni hapa nchini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: