Katika kuhitimisha semina ya kuwajengea uwezo: Sayyid Swafi awahimiza walimu wa shule za Alkafeel za wasichana waongeze juhudi na wafanyie kazi kwa vitendo waliyo soma kwenye semina hii

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ameongea na walimu wa Dini wa shule za Alkafeel, kuhusu kuongeza juhudi katika ufundishaji na kufanyia kazi kwa vitendo mambo waliyo fundishwa katika semina ili kutimiza malengo ya kutoa elimu bora kwa njia rahisi.

Ameyasema hayo alipo hudhuria kikao cha kufunga semina iliyo endeshwa na idara ya shule za Dini za Alkafeel kwa kushirikiana na kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, iliyokua na washiriki zaidi ya (100) ambao ni wahitimu wa fani mbalimbali, pia ni sehemu ya maandalizi ya mwaka ujao wa masomo. Kuhusu semina hii tumeongea na kiongozi wa idara ya taaluma Ustadh Karaar Maámuri ambaye pia ni mmoja wa wahadhiri na msimamizi wa semina, amesema kua: “Semina imefanyika kwa muda wa siku nne na ilikua na mada tofauti, ambazo ni:

  • 1- Njia bora za ufundishaji.
  • 2- Kazi ya uwalimu.
  • 3- Upotoshwaji wa maarifa.
  • 4- Malengo ya malezi na mkakati wa kila siku”.

Akaongeza kusema kua: “Kila warsha ilikua na (saa 7 za masomo) siku ya mwisho wakapewa mtihani katika masomo waliyo fundishwa, matokeo ya mtihani yalikua mazuri na yakuridhisha, miongoni mwa upekee wa semini hizi ni kuhusisha kipengele cha kupima athari zitokanazo na ufundishaji, kwa kutembelea shule za Alkafeel zilizopo katika mikoa ya kati na kusini mwa Iraq ambazo walimu wake wameshiriki katika semina hapa Karbala na kuangalia maendeleo yao”.

Mwisho wanasemina wakapewa vyeti vya ushiriki, vilikabidhiwa kwao na rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Muhammad Hassan Jabiri, na makamo rais wa kitengo cha taaluma Dokta Jaasim Ibrahimi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: