Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kinafanya mkutano na wawakilishi wake kwa ajili ya kujiandaa na ziara ya Arubaini…

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Alasiri ya Jumatano (3 Safar 1441h) sawa na (2 Oktoba 2019m), kimefanya mkutano na wawakilishi wake kutoka mikoa yote ya Iraq, kwa ajili ya kuratibu uingiaji wa mawakibu katika mkoa wa Karbala, sambamba na kujadili sekta ya utowaji wa huduma na matibabu wakati wa ziara hiyo tukufu.

Mkutano umefanyika ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya, umehudhuriwa na vikundi vya watoa huduma na vikosi vya usalama vya mkoa wa Karbala, kilifunguliwa kwa Quráni tukufu, baada ya Quráni akaongea rais wa kitengo bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan ambaye amesema kua: “Hakuna asiyejua umuhimu wa maadhimisho ya Husseiniyya katika kudumisha mafundisho ya Ahlulbait (a.s), sambamba na nafasi yake katika kutoa huduma za kibinaadamu ambazo ni sehemu ya kufanyia kazi mapinduzi ya bwana wa mashahidi (a.s), na kufuata mwenendo wake kielimu na kivitendo chini ya kauli ya mbora wa wanawake wa duniani (a.s) isemayo: (Na akafanya kututii kwetu ni utaratibu wa kitamaduni), hakika maadhimisho ya Husseiniyya ni kionganishi muhimu cha roho na Ahlulbait (a.s), pia huzingatiwa kuwa kielelezo cha kufungamana na uislamu halisi na kusimama katika mstari sahihi kati ya haki na batili, pamoja na kujitenga na utawala wa Umawiyya kwani vita kati ya milengo miwili bado inaendelea”.

Akaongeza kua: “Maadhimisho ya Husseiniyya ni muendelezo wa mwenendo ulio anzishwa na Imamu Hussein (a.s), matwaghuti wamejitahidi kuzuwia maadhimisho haya kwani yanafundisha kukataa dhula na matwaghuti, ni wajibu wetu kuonyesha picha nzuri inayo endana na utukufu wa maadhimisho haya na kufuata maelekezo kutoka kwa Maraajii wetu watukufu, na kushikamana na muongozo unaotolewa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu katika Ataba mbili tukudu Husseiniyya na Abbasiyya na wawakilishi wake wote, aidha kujiepusha na kila jambo linalo haribu picha yake na kutoa mwanya kwa maadui, wa kutukana na kutoa kasoro”.

Baada yake ukafuata ujembe wa wawakilishi wake na idara wa waadhimishaji kutoka mikoa tofauti ya Iraq, ulio wasilishwa na bwana Swalahu Alma’ruuf, akasema kua: “Kikao hiki ni muhimu sana kati ya wawakilishi na idara za mawakibu Husseiniyya, Karbala hupokea mazuwaru kutoka kila mkoa wa Iraq na kutoka dunia nzima”.

Akasisitiza kua: “Maadhimisho ya Husseiniyya ni amana kwa kila muungwana, yanasaidia kulinda Dini isiharibiwe na kupotoshwa, yampasa kila mtu kua mkweli wa nia yake na vitendo vyake katika maadhimisho haya matukufu, na mawakibu ziwe ni kielelezo cha kuthibitisha hilo sambamba na kusaidiana baina yao, pamoja na kuimarisha ulinzi na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kufanikisha ziara hii inayo hudhuriwa na mamilioni ya watu”.

Mkutano umepokea maoni mbalimbali kuhusu namna ya kutatua changamoto zinazo tokana na wingi wa mazuwaru.

Fahamu kua mkutano huu ni sehemu ya kukamilisha mikutano mingi iliyo fanywa siku za nyuma katika Ataba mbili tukufu, yote ilikua inakusudia kutoa huduma bora kwa mazuwaru wanaokuja Karbala, mkutano huu hufanywa kila mwaka kwa ajili ya kujipanga na ziara wa Arubaini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: