Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu yaweka msingi wa ramani ya dunia ya maendeleo endelevu (SDG)

Maoni katika picha
Miongoni mwa mfululizo wa hatua za kuelekea katika mlengo sahihi wa kielimu uliopangwa na muungano wa maktaba (Ifla), maktaba na daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika mkakati wake wa mpango wa maendeleo endelevu unaodumu hadi mwaka (2030m), ambapo maktaba imesha piga hatua katika (SDG) na imeweza kufanikisha yanayo hitajika katika mkakati huo.

Hayo yaliongelewa kwenye wiki ya muungano wa maktaba (Ifla) ambayo yalijadiliwa malengo ya maendeleo endelevu kwenye kongamano lililofanyika kuanzia (20 – 30 /09 /2019m), zitaonyeshwa program maalum za kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu kimataifa, katika kuangazia mambo yanayo fanywa na maktaba katika kufanikisha malengo hayo, zilionyeshwa program mbalimbali za maktaba kuelekea (SDG), na nakala kale za Atabatu Abbasiyya tukufu kama sehemu ya maktaba za kimataifa zinazo tekeleza mkakati wa malengo endelevu (2030m), harakati hizo zinahusisha mambo yafuatayo:

  • 1- Faili za waandishi wa kiiraq.
  • 2- Kuhifadhi na kulinda turathi zilizo andikwa.
  • 3- Mradi wa uwekaji namba kiiraq katika jumbe na maoni ya wanavyuo.
  • 4- Nafasi ya maktaba za Iraq katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu.
  • 5- Nafasi za maktaba za kitabibu katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu.
  • 6- Mradi wa kuanzisha selebasi za masomo katika vitengo vya elimu vya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: