Atabatu Abbasiyya tukufu imeweka utaratibu wa kupunguza msongamano katika kuingia na kutoka ndani ya haram

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kurahisisha utembeaji wa mazuwaru watukufu, Atabatu Abbasiyya imeteua milango maalum ya kuingilia na kutokea, pia imeteua milango maalum kwa ajili ya wanaume na wanawake, kufuatia wingi wa mazuwaru wanao ingia ndani ya haram hiyo saa 24 kila siku.

Halikadhalika umeteuliwa mlango wa Imamu Hassan kutumika kwa ajili ya kuingilia mawakibu zinazo kuja ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka kila kona ya dunia, na kutokea mlango wa Kibla chini ya utaratibu maalum bila kusababisha usumbufu kwa mazuwaru.

Kila mlango umeandikwa jukumu lake kwa lugha tofauti ili kuwasaidia mazuwaru, pamoja na kuweka waelekezaji ndani ya haram tukufu, wanao saidia kuwaelekeza mazuwaru milango ya kutumia.

Yote hayo ni kwa ajili ya kurahisisha ufanyaji wa ziara ya Arubaini inayo hudhuriwa na mamilioni ya watu kutoka kila sehemu ya dunia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: