Mawasiliano ya Atabatu Abbasiyya tukufu: Mtambo wa kielektronik wa kuhesabu mazuwaru unafanya kazi makini na utatoa hesabu inayo karibia uhakika halisi

Maoni katika picha
Mhandisi Farasi Abbasi Hamza kiongozi wa idara ya mawasiliano katika Atabatu Abbasiyya amesema kua: “Hakika mtambo wa kuhesabu watu wanaokuja kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), umeanza kazi tangu siku za kwanza za ziara hii na bado unaendelea kuhesabu bila kusimama usiku na mchana, matokea yake yatakua karibu sana na idadi halisi, kazi hiyo inafanyika kwa kutumia kamera za kisasa zaidi ambazo zimesaidia sana utendaji wa mtambo huo”.

Akaongeza kua: “Baada ya mafanikio tuliyo pata ndani ya miaka minne iliyopita kwa kutoa idadi iliyo kua karibu zaidi na uhalisia, mwaka huu tumejipanga kuendeleza mafanikio hayo na kuboresha zaidi kwa kuongeza vifaa kwenye barabara zote zinazo ingia Karbala, ambazo ni: barabara ya Najafu, Hilla, Bagdad, Husseiniyya na Huru, hizo ndio barabara zinazo tumiwa na idadi kubwa ya mazuwaru, pamoja na wanao ingia kuzuru malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kupitia mawakibu (misafara) au binafsi”.

Akasisitiza kua: “Kila siku tunachukua taarifa na kuziweka kwenye ripoti, kisha zitawekwe kwenye taarifa maalum na kutangazwa katika vyombo vya habari mwishoni mwa ziara kama tulivyokua tukifanya miaka ya nyuma”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: