Kitengo cha uhusiano kina nafasi kubwa Atabatu Abbasiyya katika ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Miongoni mwa vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu vyenye nafasi kubwa Atabatu Abbasiyya kwenye ziara ya Arubaini ni kitengo cha uhusiano, japo kua kazi zake hazionekani kwa macho, lakini kina umuhimu mkubwa wakati wa ziara na mwingineo pia, kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo hicho Sayyid Muiin Nasrullah.

Amesema kua: “Kitengo hiki ni kiunganishi baina ya Atabatu Abbasiyya na taasisi za nje, sawa ziwe kutoka ndani au nje ya Iraq, huweka uhusiano na ushirikiano mzuri na watu mbalimbali wanaokusudia kutembelea Ataba tukufu kutoka kila sehemu ya dunia, aidha huwasiliana na vitengo vingine vya Ataba kwa ajili ya kuandaa kila kinacho hitajiwa na wageni katika safari yao”.

Akabainisha kua: “Katika ziara hii tulifanikiwa kuwapa viza wageni wote waliokusudia kuja kutembelea Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na kuwapa huduma mbalimbali, mwaka huu tulikua na makundi ya madaktari kutoka nchi tofauti, baadhi yao walifanya kazi kwa vikundi huku wengine wakifanya kazi mmoja mmoja, bila kusahau makundi ya waandishi wa habari waliokuja kutoka nchi tofauti duniani, wote waliandaliwa sehemu za malazi zinazo endana na shughuli zao chini ya Atabatu Abbasiyya”.

Akaendelea kusema: “Ukumbi wa utawala ulikua wazi siku zote za ziara kwa ajili ya kupokea wageni, pia kuna idara nyingine inahusika na jambo hilo ambayo ni idara ya uhusiano wa vyuo, walijitolea magari ya wagonjwa na wahudumu katika vituo vya kuelekeza walio potelewa au kupotezana, pia kuna watumishi wa kitengo chetu walio saidia kuongoza misafara ya watu na mawakibu zinazo ingia na kutoka katika haram”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: