Kitengo cha utumishi kimeanza kufanya usafi ndani ya mji na kwenye barabara zinazo elekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kama kawaida baada ya kumaliza ziara ya Arubaini, kuanzia siku ya mwezi ishirini na moja Safar, watumishi wa idara ya usafi chini ya kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasiyya tukufu huanza kufanya usafi, husafisha maeneo yote ya mji mkongwe pamoja na uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.

Kiongozi wa idara ya usafi chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu na msimamizi wa usafi huo Ustadh Riyaadh Khadhiir Hassan ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Watumishi wa idara yetu wameanza kufanya usafi baada ya ziara ya Arubaini kama ilivyo zoweleka, tumewagawa katika vikundi, wanafanya kazi kwa kusaidiana na watumishi wa kujitolea waliokuja kutoka miji tofauti wapatao (400), wamesambazwa sehemu tofauti ndani ya mji mkongwe pamoja na kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu”.

Akaongeza kua: “Wanafanya kazi saa (24) kwa kutumia vifaa vya aina tofauti, hadi watakapo maliza kusafisha eneo lote la mji mkongwe, hali kadhalika watumishi wa kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili wanafanya kazi kubwa ya usafi, pamoja na watumishi wa mkoa wa Karbala”.

Akasema: “Tumesafisha pia sardabu zote za Atabatu Abbasiyya tukufu zilizo tumika kama sehemu ya kupumzika na kulala mazuwaru na wafanya kazi wa kujitolea wakati wa ziara ya Arubaini”.

Kumbuka kua idara ya usafi chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, iligawa zaidi ya vitambulisho eflu moja kwenye mawakibu tofauti wakati wa ziara ya Arubaini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: