Umuhimu wa kitengo cha usimamizi wa haram tukufu katika ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo cha usimamizi wa haram tukufu ni miongoni mwa vitengo vinavyo toa huduma ya moja kwa moja kwa mtu anayekuja kufanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), watumishi wa kitengo hicho pamoja na wale wa kujitolea waliweka mkakati maalum wa kuwahudumia mazuwaru, wamefanya kazi ya kuratibu na kusafisha miswala au kubadilisha, sambamba na kuongoza uingiaji na utokaji wa mawakibu za kuomboleza, kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo hicho bwana Nizaar Ghani Zubaidi.

Akaongeza kua: “Kitengo kilianza maandalizi ya ziara hii muda mrefu, kiliandaa mahitaji muhimu yote kwa ajili ya kupokea wageni wanaokuja kuzuru malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakaigawa haram tukufu sehemu tofauti, kwa lengo la kurahisisha uingiaji na utokaji wa mazuwaru katika haram tukufu na kuepusha msongamano, pamoja na kufanya usafi ndani ya haram wakati wa ziara na baada yake, watumishi wake wameenea kila sehemu ndani ya hara tukufu kwa ajili ya kuongoza mazuwaru wakike na wakiume”.

Akabainisha kua: “Watumishi wa kitengo hiki pia husaidia watu wenye ulemavu na wazee kufanya ziara na kusoma dua, pia huandaa sehemu za kuswalia jamaa, bila kuathiri harakati za mazuwaru, pia hupuliza marashi mazuri ndani ya haram kulingana na mazingira ya hali ya hewa, hali kadhalika wanaweka vitabu vya ziara na dua kwenye kabati za vitabu”.

Akaendelea kusema: “Watumishi wetu wapo kila mahala kwa ajili ya kusaidia mazuwaru na kujibu maswali yao, kuhusu sehemu za kuingia na kutoka pamoja na vitengo wanavyo taka kwenda, kama vile kitengo cha Dini, Mafqudaat nk. Pia wameanzisha njia maalum kwa ajili ya kurahisisha utembeaji ndani ya haram na kuzuwia msongamano”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: