Watumishi wa kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu wanafanya usafi baada ya kumaliza msimu wa ziara ya Arubaini…

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu chini ya Atabatu Husseiniyya na Abbasiyya, kama kawaida yao baada ya kuisha msimu wa ziara ya Arubaini, wameanza kusafisha uwanja wa katikati ya haram mbili na barabara zinazo elekea eneo hilo pamoja na malango ya kuingia mji mkongwe, watumishi wote wa kitengo hicho wanashiriki katika usafi huo.

Tumeongea na rais wa kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili Ustadh Naafii Mussawi kuhusu kazi hiyo, amesema kua: “Kama kawaida, kila mwaka unapo isha msimu wa ziara ya Arubaini, watumishi wetu husafisha eneo lote la katikati ya haram mbili tukufu na barabara zinazo elekea eneo hilo, pamoja na malango ya mji mkongwe”.

Akaongeza kua: “Watumishi wote wa kitengo chetu wanashiriki katika usafi huu, wakiwa na zaidi ya mitambo ya usafishaji (18) sambamba na gari zingine za usafi, hadi sasa wamesha ondoa zaidi ya tani (2500) za uchafu na kazi bado inaendelea”.

Akasema kua: “Kazi inaendelea muda wote hatuta pumzika hadi tuondoe uchafu wote katika barabara zinazo zunguka eneo la katikati ya haram mbili tukufu na kwenye malango ya kuingia mji mkongwe”.

Tambua kua kitengo cha uwanja wa katikati ya haram mbili chini ya Atabatu Husseiniyya na Abbasiyya kilifanya kazi kubwa ya kuhudumia mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), waliokuja mamilioni kwa mamilioni katika mji mtukufu wa Karbala kutoka kila sehemu ya dunia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: