Maahadi ya qur’ani tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislam na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiiyya imetoa idadi ya watu walio fikiwa katika mradi wa kufundisha usomaji sahihi kwa mazuwaru. Jumla ya watu (200,000) waliokuja kufanya ziara ya Arubaini mwaka huu 1441h wamefikiwa, vituo vya kufundishia viliwekwa kwenye mikoa tofauti na katika barabara zinazoelekea Karbala, miongoni mwa sehemu viliko wekwa vituo ni (Bagdad, Muthanna, Najafu, Baabil, wilaya ya Hindia, na mjini Karbala).
Kulikuwa na vituo zaidi ya (120) na walimu zaidi ya (500), asilimia kubwa ya wanufaika ni vijana wadogo walio kosa fursa ya kusoma pamoja na wageni kutoka mataifa mbalimbali hasa wasio ongea kiarabu. Mkuu wa maahad ya Qur’ani tukufu shekh Jawadi Nasrawi amesema kuwa: “Atabatu abbasiyya tukufu inatoa huduma nyingi kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ziara ya Arubaini, miongoni mwa huduma hizo ni kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu kwa mazuwaru, kazi hiyo famefanywa na Maahadi ya Qur’ani chini ya Ataba tukufu”.
Akasema “Mwaka huu tumewafikia zaidi ya watu (200,000), tulifungua zaidi vituo (120) kwenye mikoa tofauti na tulikua zaidi ya walimu (500), wamefanya kazi ya kufundisha usomaji sahihi wa surat Fat-ha na maneno ya kuswalia”.
Nasrawi ametoa shukrani za dhati kwa kila mtu aliye saidia kufanikiwa mradi huu, Wakiongozwa na mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi pamoja na viongozi wote wa Ataba tukufu, kufuatia faida kubwa iliyo patikana kutokana na mrazi huu kama ilivyo simuliwa na wakufunzi wa mradi pamoja na watumishi wa Maahadi na washiriki.