Kikosi cha uokozi katika idara ya uhusiano wa vyuo vikuu kimeshughulikia zaidi ya matukio (750) wakati wa ziara ya Arubaini miongoni mwao kuna waliokua katika hali mbaya

Maoni katika picha
Kikosi cha uokozi katika idara ya uhusiano, kinacho undwa na wanfunzi wa masomo ya udaktari (udaktari – uuguzi – famasia) kutoka vyo tofauti vya Iraq, kimetangaza kushughulikia zaidi ya matukio (750) wakati wa ziara ya Arubaini, wakiwemo watu waliokua katika hali mbaya zaidi, kimefanikiwa kuwavusha salama baada ya kupewa huduma walizo stahiki kwa wakati, na kufikishwa katika hospitali za karibu, hospitali ya Maidani iliyo funguliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu au hospitali ya Safiir au Husseini.

Msimamizi wa harakati za vyuo vikuu vya udaktari kwenye ziara ya Arubaini katika Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Mahmuud Qarah Ghuli, ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Jopo la wanafunzi wa udaktari kutoka vyuoni baada ya kutambua uwezo wao na kuwapa semina kadhaa za mkakati wa kutoa huduma za kimatibabu ulio pangwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, jopo la madaktari hao walichukua jukumu la kutoa huduma ndani ya magari ya wagonjwa yaliyopo katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, na kwenye barabara zinazo elekea katika eneo hilo karibu na haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Akabainisha kua:

  • - Asilimia kubwa ya watu walio okolewa ni wazee, kikosi hicho kilikua kinatoa huduma kwa haraka na kuwapeleka waathiriwa kwenye hospitali ya karibu kwa matibabu zaidi.
  • - Kila muathirika aliingizwa kwenye gari la wagonwa la karibu yake na kupelekwa hospitali.
  • - Wale waliokua katika hali mbaya sana walipelekwa katika hospitali kubwa kama vile Safiir na Husseini.
  • - Kusaidia kutoa huduma kwenye vituo vya afya na hospitali ya Maidani ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya.

Akafafanua kua: “Tulifanikiwa kuokoa, kutibu na kusafirisha makumi ya wagonjwa kila siku, walio athiriwa na msongamano mkubwa wa mazuwaru”.

Kumbuka kua harakati hizi ni miongoni mwa mkakati wa kitabibu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mazuwaru, na hushiriki vitengo tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: