Mwezi ishirini na nane ni siku ya kukumbuka kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w)

Maoni katika picha
Mwezi ishirini na nane Safar huzuni za watu wa nyumba ya Mtume (a.s) hufikia kilele.. siku hiyo inamsiba mkubwa ulio umiza roho zao na ukawa mwanzo wa majonzi kwao, siku kama ya leo mwaka wa (11 h), mbora wa viumbe na bwana wa mitume Muhammad (s.a.w.w) alifariki dunia akiwa na umri wa miaka (63).

Imamu Ali (a.s) alisimamia maziko yake na wala hakushirikiana na yeyote, alimuosha, kumvisha sanda, kumswalia na kumzika, kisha akasimama pembeni ya kaburi lake na akasema: (Hakika subira ni nzuri ispokua kwa ajili yako, kusononeka ni kubaya ispokua kwa yababu yako, msiba wako ni mkubwa, na baada yako ni kidogo).

Halafu kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s) akasema:

Baada ya kumvisha sanda mtume na kumzika ** hadi nguo zake zimeomboleza kifo chake.

Tumeondokewa na mtume wa Allah hatuta muona ** hakuna mfano wake katika walimwengu.

Akapokewa na Fatuma Zaharaa (a.s) kwa kauli yake:

Nakuambie uliye ondoka duniani ** kama unasikia sauti yangu na wito wangu.

Nimepatwa na msiba mkubwa lau kama ** ungeupata mchana ungegeuka kua usiku.

Baada yako huzuni ndio liwazo langu ** hakika kukulilia itakua ndio kazi yangu.

Itakua vipi kwa aliyenusa udongo wa Ahmadi ** tambua zama zote atanusa machungu.

Kutoka kwa Imamu Baaqir (a.s) anasema: (Ulipo fika wakati wa kufariki Mtume (s.a.w.w) alikuja Jibrilu (a.s) akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je unataka kurudi? Akasema (s.a.w.w): hapana.. nimesha fikisha ujumbe wa Mola wangu, kisha akasema: unataka kurudi duniani? Akasema (s.a.w.w): hapana.. bali nataka kwenda kwa rafiki mkuu).

Kisha Mtume (s.a.w.w) akasema kuwaambia waislamu waliokua wamemzunguka: (Enyi watu.. Hakuna mtume baada yangu, wala hakuna sunna baada ya sunna zangu, atakayedai hayo ataingia motoni, watakao dai hayo wataingia motoni.

Enyi watu pendeni kulipa kisasi na pendeni kufanya haki wala msifarakane, kuweni waislamu mtasalimika, (Mwenyezi Mungu ameandika: Hapana shaka mimi na Mtume wangu tutashinda. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu, mwenye kushinda).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: