Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Maoni katika picha
Katika kumbukumbu ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) chini ya ratiba yake maalum katika msiba huu unao umiza waislamu wote, uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya Jumapili (28 Safar 1441h) sawa na (27 Oktoba 2019m), wamefanya majlisi maalum ya kuhuisha huzuni za watu wa nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Baada ya kusomwa Quráni ya ufunguzi, Sayyid Adnani Mussawi kutoka kitengo cha Dini alipata nafasi ya kutoa mawaidha, amezungumza sifa na hadhi kubwa ya mbora wa walimwengu mtukufu Muhammad (s.a.w.w), kisha akaeleza maisha yake na mitihani aliyo pata katika kutangaza haki na kusimika misingi ya Dini ya kiislamu, aidha aka fafanua ukubwa wa pengo lake kihistoria baada ya waislamu kuondokewa na Mtume (s.a.w.w).

Majlisi ikahitimishwa kwa kaswida na mashairi ya huzuni yanayo onyesha majonzi ya waumini kwa kuondokewa na Mtume (s.a.w.w) na machungu waliyo nayo katika kuomboleza msiba huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: