Miongoni mwa juhudi za kusaidia watu wanaofanya maandamano ya amani na kudai haki zao kisheria: Atabatu Abbasiyya tukufu inagawa maelfu ya lita za maji baridi kwa waandamanaji wa Karbala

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu bado inaendelea kusaidia watu wanaofanya maandamano ya amani na kudai haki zao kisheria, zilizo tajwa katika katiba na kuungwa mkono na Marjaa Dini mkuu, miongoni mwa huduma wanazo toa kwa waandamanaji ni ugawaji wa maji baridi ya kunywa.

Idara ya maji katika Atabatu Abbasiyya tukufu, chini ya kitengo cha utumishi, imechukua jukumu la kugawa maji, kiongozi wa idara hiyo bwana Ahmadi Hanuun ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, na miongoni mwa harakati za kuunga mkono watu wanao andamana kwa amani, ikiwa pia ni sehemu ya maombi ya waandamanaji, ndipo ikaamuliwa kujibu sehemu ya maombi yao kwa kuandaa maelfu ya lita za maji sambamba na kugawa barafu pia kwa ajili ya kupozea maji yanayo wekwa kwenye madeli, tayali kwa kutumiwa na waandamanaji pamoja na askari”.

Akaongeza kua: “Kazi haijaishia hapo peke yake, bali tunagawa maelfu ya chupa za maji kutoka kwenye kiwanda cha maji Alkafeel, kazi hiyo inafanywa muda wote”.

Fahamu kua Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa huduma nyingi kwa watu wanaofanya maandamano ya amani, kama vile:

  • - Kuandaa chakula kutoka katika mgahawa wa Ataba tukufu kwenye maeneo wanayo kusanyika waandamanaji.
  • - Kugawa maelfu ya chupa za maji ya kunywa.
  • - Kugawa matunda, juisi na chai kwa nyakati tofauti.
  • - Kufanya usafi kwa kutumia gari maalumu katika maeneo yanayo tumiwa zaidi na waandamanaji.
  • - Kufungua vituo cha kugawa maji sehemu tofauti.
  • - Kutibu wananchi na askari wanao pata matatizo ya afwa wakiwa kwenye maandamano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: