Marjaa Dini mkuu: Wanasiasa waliopo madarakani wanafursa ya kutekeleza madai ya wananchi chini ya utaratibu watakao kubaliana na ndani ya muda maalum.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amebainisha kua: Wanasiasa waliopo madarakani wanafursa ya kutekeleza madai ya wananchi chini ya utaratibu watakao kubaliana na ndani ya muda maalum, wakomeshe ufisadi na watende haki, haifai kuendelea kuchelewa katika swala hili kutokana na hatari kubwa inayolikumba taifa kwa sasa.

Ameyasema hayo katika khutuba ya pili ya swala ya Ijuma leo (10 Rabiul-Awwal 1441h) sawa na (8 Novemba 2019m), iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai, ifuatayo ni nakala ya khutuba hiyo:

Enyi mabwana na mabibi.. nakusomeeni nakala iliyo tufikia kutoka ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Sistani katika mji wa Najafu Ashrafu.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

Wananchi wanaendelea kuandamana sehemu mbalimbali za nchi na kudai mabadiliko, kuna baadhi ya matukio wanayofanya yanaonyesha utukufu wa raia wa Iraq, wanasifa ya ushujaa, kujitolea, subira, msimamo na kuhurumiana baina yao, leo tunakumbuka watu wa kwanza walio fariki siku za kwanza za harakati hii kabla ya siku arubaini nyuma, Mwenyezi Mungu awarehemu, tunawakumbuka kwa kutaka wahusika wa mauwaji hayo wafikishwe kwenye vyombe vya sheria, tunazipa pole familia zao na tunaomba Mwenyezi Mungu awaponye haraka majeruhi, tunapenda kueleza nukta kadhaa:

Kwanza: Viongozi wa kisiasa waliopo madarakani wana fursa ya kutekeleza madai ya wananchi chini ya utaratibu watakao kubaliana ndani ya muda maalum, na kukomesha ufisadi na kutenda haki, wala haifai kuendelea kuchelewa katika hilo, kutokana na hatari kubwa inayo likumba taifa kwa sasa.

Pili: Kulinda usalama wa waandamanaji ni jambo muhimu sana, kwa sehemu kubwa hilo ni jukumu la vyombo vya ulinzi na usalama, wanatakiwa wajizuwie kutumia nguvu wanapo amiliana na watu wanaofanya maandamano ya amani, kwani kutumia nguvu kunamadhara makubwa. Asilimia kubwa ya waandamanaji wanafanya maandamano ya amani, hawawachokozi askari wala hawaharibu mali za umma na binafsi, yapasa kuwanasihi waandamanaji wachache ambao bado wanachokoza askari na kuharibu mali waache kufanya hivyo, ili maandamano yabakie kua ya amani yasiyokua na dosari yeyote.

Tatu: Hakika kufanya maandamano ya amani ni haki ya kila muiraq, ni njia ya kutoa maoni na kudai haki, anayetaka anaweza kushiriki na asiyetaka asishiriki, haifai kumlazimisha mtu afanye vile unavyo taka, wala haifai kushiriki au kutoshiriki iwe sababu ya watu kuanza kutuhumiana, kila mtu anatakiwa aheshimu maoni ya mwenzake, na amvumilie katika maoni yake.

Nne: Kuna milengo ya ndani na kigeni ilikua na mchango katika miongo ya nyuma kwa madhila yalilolikumba taifa la Iraq, milengo hiyo inaweza kutaka kutumia fursa hiyo leo pia kufanikisha malengo yao, yawapasa waandamanaji wachukue tahadhari kubwa ya kuhakikisha watu hao hawaleti madhara na kubadilisha muelekeo wao.

Tano: Hakika askari wetu wapenzi na wale walio ungana nao katika kupigana na Daesh pamoja na kuilinda Iraq, wana heshima kubwa kwa kila mtu, hususa wale wanaoendelea kulinda mipaka yetu hadi sasa, na vyombo vyote vya ulinzi na usalama popote walipo kutokana na jukumu kubwa walilo nalo kwa taifa hili, haifai kusahau utukufu wao, hawatakiwi kusikia neno lolote la kusemwa vibaya kutokana na jinsi wanavyo jitolea kwa ajili yetu, leo tumeweza kufanya maandamano ya amani kwa usalama kutokana na kazi yao, lazima tuwatukuze na kuwaheshimu.

Ewe Mola tusamehe dhambi zetu na utuepushe na mabaya pamoja na vitimbi vya maadui, tuongoze katika njia yako madhubuti na kamba iliyo nyooka, hakika wewe ni mwingi wa kusikia maombi na mwingi wa kujibu, kila sifa nyema inamstahiki Mola wa walimwengu, Rehema na amani ziwe juu ya Muhammad na kizazi chake watakasifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: