Kituo cha utamaduni wa familia kimeratibu mafunzo kwa taasisi ya Nuurul-Hassan Alkhiryya ya mayatima.

Maoni katika picha
Kituo cha utamduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimeratibu mafunzo kwa wakina mama wa mayatima, ambao taasisi ya Nuurul-Hassan Alkhairiyya inawahudumia, nayo ni moja ya taasisi za khairiyya katika mkoa wa Karbala, mafunzo hayo yamepewa jina la: (mahitaji ya kinafsi kwa vijana), yanalenga kuongeza uwelewa wa wakina mama kuhusu namna ya kuamiliana na vijana.

Mafunzo hayo yanasimamiwa na kuratibiwa na mtaalamu mwenye uzowefu mkubwa kwenye sekta hiyo, anauwezo wa kuamiliana na tatizo lolote sambamba na kulitafutia ufumbuzi. Kiongozi wa kituo tajwa Ustadhat Asmahani Ibrahim ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Bado tunaendelea na ratiba yetu inayo lenga kusaidia kujenga uwelewa wa wakina mama kuhusu namna ya kuamiliana na vijana, nayo ni moja ya ratiba zinazo tekelezwa na kituo, katika ratiba hii kuna vipengele vingi, zikiwemo njia za kuamiliana na vijana, wamefundishwa mada nyingi zinazo endana na mazingira halisi tunayo ishi pamoja na mifano hai, na kuonyeshwa njia za kutatua changamoto mbalimbali”.

Akaongeza kua: “Kulikua na kipindi cha maswali na majibu, pamoja na kuwaonyesha namna ya kutatua changamoto kwa kutumia mbinu za kisasa kulingana na aina ya changamoto”.

Akasisitiza kua: “Mafunzo haya yanamwitikio mkubwa na mahudhurio mazuri, kutokana na urahisi wa kuelewa mambo yanayo someshwa na umuhimu wake kwa wahusika”.

Kumbuka kua kituo kilitoa wito kwa wakinamama wanaopenda kushiriki kwenye mradi huu, wawasiliane nasi kwa simu namba (07828884555) au kupitia mitandao ya kijamii (Viber, Whatsap, Telegram), au kujiunga katika kituo cha utamaduni wa familia kupitia linki ifuatayo: https://t.me/thaqafaasria1
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: