Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Najafu inafanya semina kuhusu matamshi ya herufi na sifa zake.

Maoni katika picha
Semina za Quráni zinazo endeshwa na kusimamiwa na Maahadi ya Quráni katika Atabatu Abbasiyya tawi la Najafu bado zinaendelea, wameandaa semina kuhusu matamshi na sifa za herufi, semina hii ni sehemu ya kukamilisha semina zilizo tangulia zinazo lenga kutoa wasomi bora na walimu wenye uwezo mkubwa.

Mkufunzi wa semina hii ni Dokta Karim Zubaidi, anafundisha misingi ya usomaji wa Quráni tukufu na kuipa kila herufi haki yake na kulinda ulimi usikosee wakati wa kusoma, ni somo linalohusu maneno ya Quráni na herufi zake sambamba na kuhakikisha zinatamkwa kwa ufasaha, washiriki wanasomeshwa kwa nadhariyya na vitendo.

Ratiba ya semina hii wanasomeshwa siku mbili katika kila wiki, kwa muda wa saa mbili kila siku na inahudhuriwa na idadi kubwa ya wasomi wa Quráni na wapenzi wa maneno ya Mwenyezi Mungu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: