Kamati ya maandalizi ya kongamano la kimataifa kuhusu maarifa ya Qur’ani na manhaji za tafsiri baina ya hali ya zamani na sasa yatoa wito kwa wasomi na watafiti waje kushiriki.

Maoni katika picha
Katika kukamilisha mfululizo wa makongamano ya kielimu yanayo julikana kwa jina la (Hauza ni kitovu cha mabadiliko) yanayo fanywa kwa ushirikianao kati ya Atabatu Abbasiyya na taasisi ya Bahrul-Uluum Alkhairiyya, kamati ya maandalizi imeandaa awamu ya tano yenye anuani isemayo: (Kongamano la kimataifa kuhusu maarifa ya Qur’ani na manhaji za tafsiri baina ya hali ya zamani na sasa) litakalo fanyika tarehe (4 – 6 machi 2020m), na kutoa wito kwa wasoni na watafiti wa Quráni waje kushiriki chini ya mada zifuatazo:

  1. Nafasi ya (wanachuoni wa hauza) katika:

  • Kubainisha aina za miujiza ya Quráni.
  • Kulinda Quráni tukufu na kuondoa utata kuhusu Quráni.
  • Kuandika kuhusu tafiti za maarifa ya Quráni na tafsiri zao.
  • Ukosoaji wa manhaji ya tafsiri ya Quráni.
  • Kurahisisha ujifunzaji wa Qur’ni kwa wasio ongea kiarabu.

  1. Nafasi yao katika utumishi.

  • Aya za Quráni katika kutoa hukumu za kisheria.
  • Elimu za lugha ya kiarabu na adabu zake pamoja na (elimu saidizi) katika kutafsiri aya za Quráni na kuzifanyia ta-awiil.
  • Masomo ya usulu katika tafsiri ya Quráni na ta-awiil.
  • Aya za Quráni katika kulinda Aqida.
  • Aya za Quráni katika kutatua changamoto za jamii.

  1. Msimamo wao katika:

  • Uhusiano kati ya tafsiri ya aya ya Quráni na ta-awiil.
  • Swala la majazi katika Quráni.
  • Swala la historia ya Quráni.
  • Kusoma Quráni kwa taratibu mpya na kulinganisha.
  • Utafiti wa Mustashrikina na Mustaghribina katika Quráni.

  1. Juhudi za wanachuoni wa hauza na wa sekula kuhusu Quráni.

Amma kuhusu masharti ni:

  • 1- Utafiti usiwe umesha wahi kutolewa mahala pengine.
  • 2- Utafiti uwe na mashiko yanayo kubalika kielimu na sio visa vya kutunga.
  • 3- Utafiti utokane na mada zilizo tajwa.
  • 4- Izingatiwe misingi ya kielimu katika uandishi wa utafiti.
  • 5- Kamati haiwajibiki kurudisha utafiti kwa muandishi wake sawa umekubaliwa au haujakubaliwa.
  • 6- Tafiti zote zitawasilishwa mbele ya jopo la majaji na kuzishindanisha kielimu.
  • 7- Utafiti uandikwe katika karatasi ya (A4) na kuhifadhiwa kwenye (CD) usizidi kurasa 25, maandishi yawe na ukubwa wa saizi 14 na hamishi ya saizi 12 hati ya (Simplified Arabic).
  • 8- Utafiti uambatanishwe na wasifu wa mundishi kielimu (cv) pamoja na namba ya simu na anuani ya barua pepe.
  • 9- Mwisho wa kupokea tafiti ni (1 /2/ 2020m).

Tafiti zitumwe kupitia barua pepe ya kongamano (Alhawza.36@gmail.com) au kupitia telegram kwa namba ya simu (+9647703888288).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: