Kitengo cha miradi ya kihandisi imemaliza kazi ya kufanyia matengenezo vituo vya kusafisha maji vilivyo jengwa na Atabatu Abbasiyya katika maeneo mbalimbali.

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu inamiradi mingi ya kutoa huduma, miongoni mwa miradi hiyo ipo inayomgusa mwananchi moja kwa moja, imetumia uwezo wake wote kupunguza changamoto za raia, miongoni mwa changamoto kubwa ambayo kitengo hiki kimeifanyia kazi na kusaidia kuitatua ni tatizo la maji, Atabatu Abbasiyya imejenga vituo vya kusambaza maji (R.O station) katika maeneo mbalimbali, idadi ya wanufaika wa mradi huu ni maelfu kwa maelfu pamoja na mazuwaru na mawakibu, kuna baadhi ya vituo vilianzishwa rasmi kwa ajili ya kuwahudumia mazuwaru ndani na nje ya mkoa wa Karbala.

Kwa ajili ya kuhakikisha vituo hivyo vinadumu, kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia wataalamu wake wa idara ya maji, hufanya matengenezo kila baada ya muda fulani chini ya utaratibu maalum, huandaa timu ya mafundi kwa ajili ya kukarabati vituo hivyo, tumeongea na mkuu wa idara ya maji Mhandisi Ahmadi Amjadi Husseini amesema kua: “Vituo vyoto hufanyiwa matengenezo kila baada ya muda fulani chini ya utartibu uliopangwa, na kuhakikisha vinaendelea kusambaza maji kwa ukamilifu”.

Akaongeza kua: “Kazi zimegawanyika sehemu mbili, kwanza ni ukarabati wa mitambo ya kusambaza maji na pili ni kufanya uboreshaji kwa kuweka vifaa vya ziada, kwa ajili ya kuongeza uzalishaji, miongoni mwa marekebisho hayo ni:

  • - Kukarabati mitambo ya kusukuma maji.
  • - Kufanyia matengenezo vituo vya kusafisha maji (RO) na kubadilisha vifaa vilivyo choka.
  • - Kukarabati mabomba yanayo tumika kusukuma maji na kuhakikisha maji yanapita vizuri ndani ya mabomba hayo.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya inamiradi mingi ikiwemo ambayo inamgusa moja kwa moja mwananchi wa Iraq, imejitahidi kupunguza changamoto za wananchi kadri ya uwezo wake, miongoni mwa miradi muhimu ni huu wa maji, jumla ya vutuo (20) vya kusambaza maji (R.O station) vimejengwa na Atabatu Abbasiyya katika sehemu mbalimbali, maelfu kwa maelfu ya watu wamenufaika na mradi huu, pamoja na mazuwaru na mawakibu, kuna vituo vilivyo anzishwa rasmi kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru na mawakibu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: