Muhimu na hivi punde.. Majraa Dini mkuu ameendelea kusisitiza maandamano ya amani na utukufu wa damu ya muiraq.

Maoni katika picha
Muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu kwenye khutuba ya Ijumaa ya leo (24 Rabiul-Awwal 1441h) sawa na (22 Novemba 2019m) ndani ya haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) amesoma nakala kutoka ofisi ya Marjaa Dini mkuu huko Najafu.

Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai amesema kua: Enyi mabwana na mabibi.. nakusomeeni nakala iliyotufikia kutoka katika ofisi ya Mheshimiwa Ayatullahi Sayyid Sistani katika mji wa Najafu, inasema kua:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

Hakika Marjaa Dini mkuu amesha eleza msimamo wake kuhusu maandamano ya amani ya kudai islahi kwenye khutuba za Ijumaa zilizo pita na kufafanua nukta kadhaa kuhusu maandamano hayo, alisisitiza sana maandamano yawe ya amani, yasisababishe uvunjifu wa amani wala uharibifu wa mali, na anaendelea kusisitiza jambo hilo, aidha ansisitiza umuhimu wa kumaliza haraka uandaaji wa kanuni za uchaguzi na ugombeaji, kwa namna ambayo ilitajwa katika khutuba za nyuma, jambo hilo litasaidia kutuvusha kwenye matatizo makubwa tunayopitia kama taifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: