Haifai kusahau utukufu wao.. idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inasaidia waandamanaji na inaendelea kusaidia wapiganaji waliopo kambini.

Maoni katika picha
Pamoja na mazingira magumu ya taifa kwa sasa kutokana na maandamano ya kudai haki za kisheria, idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu haijawasahau wapiganaji waliopo kambini, inasaidia sehemu zote mbili: insaidia waandamanaji waliopo katika viwanja vya maandamano kwenye mikoa mbalimbali ya Iraq, sambamba na kuendelea kusaidia wapiganaji chakula na vitu vingine, kwa namna ambayo inawapa nguvu ya kupambana na kila atakayetaka kuharibu amani ya Iraq, misaada hiyo ni sehemu ya kufanyia kazi agizo la Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Sistani alilotoa hivi karibuni, pale alipo sema (…Haifai kusahau utukufu wao, hawatakiwi kusikia neno lolote la kuwavunjia heshima kutokana na jinsi walivyo jitolea, leo tumeweza kufanya maandamano na makongamano makubwa bila kuwa na hofu ya kushambuliwa na magaidi kutokana na kazi kubwa wanayo fanya majemedali hao, wanatakiwa kuheshimiwa na kutukuzwa).

Ofisi ya Bagdad (Labbaika ewe Iraq/ Ukoo wa Sudani) chini ya idara ya ustawi wa jamii imeandaa msafara chini ya kauli mbiu isemayo (Hashdi wana haki kwetu), msafara huo umeelekea katika kambi za wapiganaji mkoani Mosul, kwa mujibu wa maelezo ya Shekh Tahsiin Sudani naibu kiongozi wa ofisi ya Bagdad/ Karkhi, akaongeza kua: “Hakika msafara huu ni sehemu ya misafara mingi iliyo kwenda sehemu tofauti za kambi za wapiganaji, tumewasili kwa wapiganaji wa mji wa Hadhar, wapiganaji wa Liwaau Answari Marjaiyya/ 44 Hashdi Shaábi, tukiwa na aina mbalimbali za vyakula na matunda pamoja na vyakula vikavu, kwa ajili ya kuwashajihisha kulinda ushindi uliopatikana kwa utukufu wa damu za mashahidi wa jeshi la serikali na Hashdi Shaábi”.

Kikosi cha ustawi wa jamii kutoka kwenye Husseiniyya ya Aali Yaasin kimechukua jukumu la kusaidia vikosi vya wapiganaji kuanzia pembezoni mwa mji wa Bagdad kusini hadi pembezoni mwa mji wa Karbala, kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa kikosi hicho Wasam Kinani, akasema: “kimetoa msaada kwa wapiganaji wa Liwaau Qahaar na Liwaau Thaqalain kwenye eneo la vikosi vya Latwifiyya, na Liwaau Mussa Alkadhim (a.s) katika mji wa Bahiraat na kikosi cha Battaar katika mji wa Huur Hussein na Liwaau Fidaau Hujjat katika eneo la Bahbaani, wametoa aina mbalimbali za chakula kilicho pikwa na kibichi”.

Wapiganaji wameshukuru sana idara ya ustawi wa amii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kutokana na kuendelea kuwasaidia wakati wote bila kuchoka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: