Shule za Al-Ameed zawapa semina ya (mental) wafanyakazi wake wanaojua kiengereza…

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kuboresha uwezo wa watumishi katika lugha ya kiengereza, jambo lenye matokea chanya katika ufundishaji wa shule za Al-Ameed, kamati ya watalamu wa lugha ya kiengereza imeandaa semina ya kutambulisha program ya (mental).

Hiyo ni program muhimu ya lugha ya kiengereza, inafundisha matumizi ya maneno mengi yanayo tumika katika shule za msingi kwa njia ya kisasa, inasaidia kuelewa lugha ya kiengereza kwa haraka.

Ustadhat Nadiya Saamir rais wa kamati ya lugha ya kiengereza amesema kua: “Warsha imehusisha walimu wa kiume na wakike, wamefafanuliwa malengo ya program na namna ya kuitumia”, akasema kua: “Warsha hii ni mwanzo wa warsha zingine zitakazo endelea siku za mbele Insha-Allah, kwa ajili ya kuendelea kuwajengea uwezo wa kutumia program hii walimu”.

Kumbuka kua shule za Al-Ameed zinamkakati wa kuboresha elimu na uwezo wa walimu wake katika sekta mbalimbali, huandaa warsha na semina mbalimbali kwa watumishi wake.

Kwa maelezo zaidi angalia katika link ifuatayo: http://alameed.iq/.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: