Kwa mara ya tatu: Watumishi wa Ataba mbili tukufu wanafanya maandamano makubwa ya amani.

Maoni katika picha
Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kwa mara ya tatu ndani ya mwezi huu, wameungana na watu wanaofanya maandamano ya amani katika mikoa mbalimbali ya Iraq, kudai haki walizopewa kisheria na kuungwa mkono na Marjaa Dini mkuu.

Maandamano yameanzia katika mlango wa Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi katika haram ya Abu Abdullahi Hussein (a.s), ambapo watumishi wa haram hiyo wakajiunga kwenye maandamano, halafu kwa pamoja wakaelekea kwenye uwanja wa maandamano kwa kutumia barabara ya Kibla, huku wakiwa wamebeba mabango yanayo dai mabadiliko ya sharia za uchaguzi na kupinga ufisadi uliojaa katika taasisi za serikali, waandamanaji wamehimiza kua maandamano ni ya amani na wanajitahidi kutofanya uharibifu wowote wa mali za umma na binafsi.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa misaada kadhaa kwa waandamaniaji, miongoni mwa misaada hiyo ni:

  • - Kuandaa chakula katika mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kwenda kukigawa kwa waandamanaji kwa kutumia gari maalum.
  • - Kugawa maelfu wa chupa za maji wa kunywa.
  • - Kugawa juisi, matunda na chai kwa nyakati tofauti.
  • - Kufanya usafi katika maeneo yanayo tumiwa na waandamanaji kwa kutumia gari maalumu za usafi.
  • - Kufungua vituo vya kugawa maji kwa waandmanaji pembezoni mwa uwanja wa maandamano.
  • - Kutoa matibabu bure kwa watu wanaopata matatizo ya afya kwenye maandamano miongoni mwa raia na askari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: