Mradi wa jengo la shule ya kufundisha turathi za Ahlulbait (a.s) kwa watoto umepiga hatua kubwa.

Maoni katika picha
Kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kuwa kiwango cha ukamilifu katika mradi wa ujenzi wa shule ya kufundisha turathi za Ahlulbait (a.s) kwa watoto umekamilikwa kwa asilimia (%90), wakasisitiza kua ujenzi huu ni mafanikio makubwa ukilinganisha na malengo ya ujenzi huo na namna unavyo tekelezwa.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo hicho Mhandisi Samiir, amesema: “Mradi huu unajengwa katika mtaa wa Baladiyya katikati ya mji wa Karbala, ni moja ya miradi mingi inayo tekelezwa na kitengo hiki bila kutegemea msaada wowote kutoka nje, kuanzia kwenye michoro hadi ujenzi pamoja na mifumo yote ya ndani”.

Akaongeza kua: “Watumishi na mafundi wanafanya kazi kubwa kuhakikisha wanakamilisha mradi huu ndani ya muda uliopangwa, mradi unajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (400) ni jengo la ghorofa mbili, kila ghorofa linakumbi (5) za darasa zilizo fungwa vifaa vya kisasa kabisa”.

Kumbuka kua mradi wa kuwafundisha watoto turathi za Ahlulbait (a.s) ni moja ya miradi ya kitamaduni chini ya shule ya Darul-Ilmi, ambayo makao makuu yake ni Atabatu Abbasiyya, unalenga kujenga uwelewa kwa watoto kuhusu turathi hizo adhim, pamoja na mambo mengine mengi na yote yanafundishwa kwa mfumo wa kisasa unao eleweka kwa urahisi na kila mtoto, hapo awali misikiti na husseiniyya zilikua zinatumika kama sehemu za kufundishia, baada ya kuongezeka kwa wanafunzi na mwitikio kuwa mkubwa ndipo likaja wazo la kujenga shule hii.

Kumbuka kua kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinawajibika na kazi za ujenzi, ukarabati na maandalizi, ndani na nje ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: