Kitengo cha malezi na elimu kinatoa zawadi kwa walimu walio faulisha kwa asilimia (%100) katika mitihani ya wizara na chawahimiza kuongeza bidii.

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinatoa zawadi kwa walimu wa shule ya wavulana Nurul-Abbasi (a.s), walio faulishwa kwa asilimia (%100) katika mtihani wa wizara wa mwaka wa masomo ulio isha katika darasa la sita na kidato cha tatu, kutokana na ufaulu huo shule yao imekua miogoni mwa shule bora katika mkoa mtukufu wa Karbala.

Wamepewa zawadi kama sehemu ya kuwashajihisha waendelee kujituma zaidi na kuendelea kushika nafasi ya ubora.

Zawadi zimekabidhiwa na Dokta Mushtaqu Ali na Ustadh Haitham Twaaiy, na kuwataka waendelee kujituma ili miaka ijayo waendelee kuwa bora zaidi.

Kwa upande wa walimu waliopewa zawadi wamesema kua, zawadi hizo zinawajenga na kuwapa moyo wa kufanya vizuri zaidi, kwa ajili ya kuandaa kizazi cha wasomi wenye uwezo wa kulinda taifa lao kielimu, kidini na kijamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: