Shughuli za uombolezaji zashuhudiwa katika Atabatu Abbasiyya tukufu kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Swidiiqah Twahirah (a.s).

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kifo cha mbora wa wanawake Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya kwanza, chini ya ratiba maalum ya kuomboleza msiba huo, Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya leo Alkhamisi (8 Rabiul-Thani 1441h) sawa na (5 Desemba 2019m) imefanya majlisi maalum kwa wafanyakazi wake ndani ya ukumbi wa utawala, ni utamaduni wa Ataba kuomboleza vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s).

Mzungumzaji alikua ni Mheshimiwa Shekh Majidi Sultani, kazungumzia utukufu wa Zaharaa (a.s) na nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya baba yake (s.a.w.w), kisha akaeleza kisa cha kifo chake, majlisi ikahitimishwa kwa kaswida iliyo amsha hisia za huzuni kutokana na msiba huu uumizao.

Shughuli za uombolezaji bado zinaendelea katika Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya hapo ikafanyika majlisi nyingine ya kuomboleza ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), muhadhiri wa majlisi hiyo akawa ni Shekh Ali Mujaan kutoka kitengo cha Dini, baada ya kusoma aya tukufu ya Quráni akazungumzia dhulma alizo fanyiwa Zaharaa (a.s), haikushambuliwa nyumba peke yake, bali alinyangánywa haki ya shamba la Fadak na ukhalifa wa mume wake kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), majlisi ikahitimishwa kwa kusoma tenzi zinazo elezea msiba huu mchungu.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu ilikua imesha andaa ratiba maalum ya kuomboleza msiba huu, unao huishwa na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kila sehemu ya dunia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: