Kwa nyoyo zenye huzuni na majonzi makubwa, watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wameimba tenzi za kuomboleza, na kumpa pole bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na Hujjat bun Hassan (a.f), katika kumbukumbu ya kifo cha mbora wa wanawake wa ulimwenguni Swidiiqah Twahirah Fatuma Zaharaa (a.s), baada ya Adhuhuri ya leo (8 Rabiul-Thani 1441h) sawa na (5 Desemba 2019m) yamefanyika matembezi ya kuomboleza ya pamoja kati ya Ataba mbili tukufu, kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha bibi Batuli (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya kwanza, iliyo taja kuwa alikufa baada ya siku arubaini toka kufariki baba yake (s.a.w.w).
Kama kawaida matembezi yameanzia ndani ya ukumbi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya watumishi wake kusimama kwa mistari na kuimba tenzi za kuomboleza, kisha wakaanza kutembea kuelekea kwenye malalo ya bwana wa mashahidi (a.s) kwa kupitia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu huki wakipiga matam, hadi walipo fika katika haram ya Imamu Hussein (a.s), wakapokewa na ndugu zao watumishi wa Abul-Ahraar (a.s) na kuungana pamoja katika uombolezaji, wakafanya majlisi ya pamoja ndani ya haram hiyo na mazuwaru waliokuwepo eneo hilo pia wakashiriki.