(Tafsiri ya Rabiu bun Anasi Albaswariy) baada ya kuhakikiwa na kuchapishwa upya.

Maoni katika picha
Baada ya kufanyiwa uhakiki na kuchapishwa upya na kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kitabu cha (Tafsiri ya Rabiu bun Anasi Albaswariy aliyefariki mwaka wa 139h), miongoni mwa ukusanyaji na uhakiki wa Dokta Nizaar Abdulmuhsin Almansuuri, kimechapishwa katika kiwanda cha Darul-Kafeel cha uchapishaji na usambazaji.

Kitabu hiki kimekusanya kazi za mwanachuoni huyo Albaswariy, pamoja na kuangazia rai zake katika kutafsiri baadhi ya aya za Quráni tukufu, naye ni miongoni mwa wafasiri wa Quráni wa kwanza, ambaye alikusanya hadithi za tafsiri ya Quráni kupitia riwaya za Ibun Abbasi na wengine.

Rabiu bun Anasi ni taabii kutoka Basra, ni mfasiri na mkusanyaji wa hadithi, hadithi alizo kusanya zipo katika vitabu vikubwa vine, alifariki mwaka wa 139h, huitwa: Alhanafiy, Albaswariy na Alkhurasaniy, alipokea kutoka kwa Anasi bun Maliki na Abu Aaliyah na Hassan Albaswariy, na akapokea kwa njia ya mursali kutoka kwa Ummu Salama na Abu Jafari Razi na Aámashi pamoja na Muqaatil bun Hayaan na wengineo, Hajaliy na Abu Haatim Swaduuq na ibun Muiin wanasema: alikua anaonyesha ushia. ametajwa na ibun Habbaan katika thiqaat, alifariki mwaka wa (139 au 140h).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: