Atabatu Abbasiyya tukufu yakabidhi bendera ya kubba tukufu kwenye makumbusho ya bendera katika chuo kikuu cha Kufa

Maoni katika picha
Ujumbe kutoka idara ya mahusiano na vyuo vikuu chini ya kitengo kikuu cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya, umekabidhi bendera ya kubba tukufu la haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) –nyeusi na nyekundu-, kwenye makumbusho ya bendera katika chuo kikuu cha Kufa, baada ya makumbusho hayo kuomba bendera hizo kwa Atabatu Abbasiyya.

Ujumbe huo umeonyesha harakati muhimu zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya katika vyuo vya Iraq, na msaada wake endelevu katika kufadhili makongamano ya kielimu yanayo nufaisha jamii, sambamba na harakati zinazo nufaisha wanafunzi wa vyuo, ujumbe huo umempongeza rais wa chuo Dokta Yaasir Lufta Hasuun kwa kupewa madaraka ya urais wa chuo kikuu cha Kufa.

Naye rais wa chuo ameonyesha utayari wake wa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya katika shughuli na harakati zinazo fanywa na idara ya mahusiano na vyuo vikuu katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Yote haya ni matunda ya harakati endelevu zinazo fanywa na idara ya mahusiano na vyio vikuu za kujenga ushirikiano kati ya Atabatu Abbasiyya na vyuo pamoja na Maahadi za Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: