Muhimu na hivi bunde.. Nakala ya tamko la Marjaa Dini mkuu kuhusu hali ya taifa la Iraq kwa sasa.

Maoni katika picha
Muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa leo (23 Rabiul-Aakhar 1441h) sawa na (20 Desemba 2019m) iliyo swaliwa ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) amesoma nakala ya tamko la Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu.

Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai amesema:

Mabwana na mabibi nakusomeeni nakala iliyo tufikia kutoka ofisi ya Mheshimiwa Ayalatullah Sayyid Sistani katika mji wa Najafu:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

Bado taifa linaishi katika mazingira magumu, bado kuna makundi ya watu yanaendelea kushiriki kwenye maandamano ya amani ya kudai islahi, huku watu wengine wakitekwa na kupewa vitisho, na upande mwingine ofisi nyingi za serikali na taasisi za elimu zinalazimishwa kufunga milango bila kuwepo na ulazima wa kufanya hivyo, huku mali za baadhi ya raia zikichomwa na kuharibiwa, watu wengi wanalalamikia udhaifu wa vyombo vya dola na baadhi ya watu kujiona wako juu ya sheria kwa hiyo wanafanya jambo lolote bila uoga.

Katika khutuba ya kwanza tumesema kua wananchi ndio msingi wa utawala na uhalali wa serikali unategemea wao –kama ilivyo kwenye katiba-, kwa hiyo njia salama ya kututoa kwenye matatizo tuliyo nayo na yanayo weza kusababisha vita ya ndani –Allah atuepushie- ni kurudi kwa wananchi, kwa kufanya uchaguzi wa mapema na kuweka sheria na kanuni zitakazo wezesha kuwa na uchaguzi huru na wa haki, sambamba na kuwa na wasimamizi huru katika ngazi zote ili kurudisha uwaminifu wa uchaguzi.

Lakini tunaona ucheleweshwaji wa kutunga kanuni za uchaguzi hadi leo, bado wabunge wanatofautiana katika mambo ya msingi, tunasisitiza tena umuhimu wa kufanya haraka kupitisha kanuni za uchaguzi tena ziendane na madai ya wananchi, zitakazo wawezesha kufanya uchaguzi huru na wa haki, kanuni hizo zinatakiwa zitukwamue katika matatizo tuliyo nayo.

Kazi ya kuandaa kanuni ikikamilika itafuata hatua ya kuchagua wanasisa wazalendo, na kupanga safu ya watu madhubuti watakao weza kuleta maendeleo ya taifa na kumaliza matatizo tuliyo nayo, kisha zifanyike kampeni za ustaarabu wala sio za kutukanana au ubaguzi wa kivyama, miji, koo au madhehebu, bali wagombea wajinadi kwa sifa zao kielimu na kiweledi sambamba na mikakati watakayo kuja nayo ya kuliondoa taifa katika matatizo tuliyo nayo na kulifikisha mahala bora, tunatarajia bunge lijalo na serikali yake ifanye marekebisho muhimu ya kulitoa taifa kwenye makucha ya ufisadi, upendeleo na kukosekana kwa uadilifu.

Mwisho ni matarajio yetu kua isichelewe sana kuundwa serikali mpya, ambayo lazima iwe tofauti na serikali zilizo pita, iwe serikali inayo endana na wakati tulio nao, itakayo rudisha haiba ya dola na kutuliza hali, na uchaguzi ujao ufanyike katika mazingira ya amani na utulivu, serikali isiyo athiriwa na watu wa nje kwa siraha wala mali na isiyo tegemea kuamuliwa mambo yake na watu wa nje.

Na Mwenyezi Mungu ni mkuu wa kuwafikisha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: