Kiwanda cha kuchapisha madaftari katika kituo cha uchapishaji na usambazaji Darul-Kafeel: tunaweza kujitosheleza kwa uzalishaji wetu wa ndani.

Maoni katika picha
Kituo cha uchapishaji na usambazaji Darul-Kafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimesema kua, kinaweza kuzalisha daftari zinazo kidhi mahitaji ya taifa, na kulifanya taifa lisitegemee madaftari kutoka nje ya nchi, jambo ambalo ni mzigo kwa taifa la Iraq na limepelekea soko kujaa madaftari yasiyokua na viwango vizuri, ambayo yameligharimu taifa pesa nyingi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wazazi na walezi.

Mkuu wa kiwanda Ustadh Farasi Ibrahimi ameongea na mtandao wa kimataifa Alkafeel kuhusu kiwanda hicho, amesema kua: “Kiwanda cha kutengeneza daftari kina hatua zote, kuanzia mwanzo kabisa wa mchakato wa kutengeneza karatasi na kuzipiga mistari, kuzikata, kuzikusanya, kuzibana na kuziwekea jalada. Kila siku tunatengeneza daftari laki moja (100,000) zenye ubora mkubwa kwa kasi ya daftari (502) kwa dakika, kiwanda chetu kina wasifu ufuatao:

  • 1- Kinaweza kuzalisha daftari za ukubwa tofauti na aina mbalimbali (kiarabu, kiengereza, kifarnsa na kihindi) kutegemea mahitaji ya mteja.
  • 2- Karatasi ni nzuri na rafiki kwa mazingira.
  • 3- Zinafunuka kwa urahisi na zinaandikika vizuri.
  • 4- Rangi zake ni imara na haziumizi macho.
  • 5- Muonekano wake unavutia na zinaumbo zuri.
  • 6- Kiwanda cha kiiraq kinacho changia katika pato la taifa.
  • 7- Bei zake rahisi tofauti na daftari zingine zilizopo sokoni.
  • 8- Kiwanda cha ndani kinauwezo wa kuhimili ushindani wa bei na kinasaidia kuacha kuagiza madaftari nje ya nchi.
  • 9- Kuna aina mbili za majalada: laini na magum”.

Akafafanua kua: “Kiwanda hakizalishi daftari peke yake, kinazalisha pia karatasi zinazo tumika kwenye machapisho tofauti na kwa ukubwa mbalimbali (A4. A3, A5, A6) zenye mistari na zisizokua na mistari”.

Akasisitiza kua: “Kiwanda chetu kinaweza kukidhi mahitaji ya wizara ya malezi na elimu ya Iraq pamoja na soko la ndani kwa ujumla”.

Kwa maelezo zaidi kuhusu kiwanda hiki tembelea sehemu kilipo katika mkoa wa Karbala –Ibrahimiyya- kituo cha Saqaa/2, karibu na kituo cha luninga ya Karbala.

Au piga simu namba: (07823950890 / 07706733834 / 07602335433) au tuandikie kupitia barua pepe ifuatayo: dar-alkafeel@outlook.com. Au tembelea toghuti yetu: https://alkafeel.net/videos/watch?key=8ba12593.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: