Kitivo cha uuguzi kimeandaa warsha ya kutambulisha chanjo katika chuo kikuu cha Al-Ameed.

Maoni katika picha
Kinga zijulikanazo kama chanjo ni msingi wa afya ya mwanaadamu kwa ujumla, humlinda mtu na maradhi hatari, kutokana na umuhimu huo kitivo cha uuguzi katika chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, kimeandaa warsha katika moja ya vituo vya afya kwenye mtaa wa Alwafaa ndani ya mji mtukufu wa Karbala.

Warsha inazungumzia chanjo na umuhimu wake kwa watoto wa chini ya miaka mitano na wakina mama wajawazito.

Watoa mada katika warsha hiyo ni walimu wa chuo cha Al-Ameed na wamefundisha mada nyingi, ikiwa ni pamoja na mada ya umuhimu wa chanjo, taratibu za kuwafanyia chanjo watoto na makosa ambayo hutokea, hususan wakati wa kuwapa chanjo watoto wenye miaka chini ya mitano, sambamba na kutoa vipeperushi vya maelezo kuhusu afya kwa ajili ya kuongeza uwelewa wa raia katika swala hilo.

Fahamu kua vitivo vilivyo chini ya chuo kikuu cha Al-Ameed ni: (udaktari – uuguzi – famasiyya – meno) vinafanya na kusimamia harakati mbalimbali zinazo lenga kuongeza uwelewa wa maswala ya afya katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: