Kwa ushiriki wa walimu hamsini (50) kutoka Baabil: kongamano la kitamaduni Alqamar limemaliza semina yake ya kumi na nane.

Maoni katika picha
Multaqa-Alqamar inayo simamiwa na kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kushirikiana na idara ya mahusiano na vyuo vikuu imeandaa kongamano la kumi na nane lililo hudhuriwa na walimu hamsini (50) kutoka Baabil. Kongamano hilo limefanyika kwa muda wa siku tatu, zimewasilishwa mada za kielimu kiimani na kimazingira.

Ustadh Farasi Shimri –mmoja wa wakufunzi kwenye kongamano hilo- amesema kua: Awamu ya kumi na nane ya kongamano hili ni mahsusi kwa walimu wa Baabil, mihadhara imetolewa na walimu wenye uzowefu mkubwa pamoja na mashekh watukufu, baada ya mhadhara wa ufunguzi na makaribisho ukafuata muhadhara wa kidini chini ya anuani isemayo (Kushikamana na Dini), halafu ukafuata muhadhara wa (fani za mawasiliano), na mhadhara wa (jifunze harakati na mwalimu mwenye mafanikio)”.

Akaongeza kua: “Ratiba ilihusisha kutembelea malalo mbili tukufu, ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), sambamba na kutembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya na kuangalia filamu ya (Ruzoba) iliyo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Washiriki wa semina wameushukuru uongozi mkuu wa Ataba tukufu, wamesema kua wamejifunza changamoto za kijamii na namna ya uzitatua kwa kushirikiana na Ataba tukufu.

Kumbuka kua kongamano la Multaqa-Alqamar ni la kitamaduni linalo lenga watu wa tabaka tofauti katika jamii, sambamba na kuangazia namna ya kupambana na changamoto za kijamii, kwa kutumia njia za kisasa bila chuki na vurugu, vitu ambavyo huleta ugonvi katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: