Baada ya miaka miwili ya ushindi: karibu dinari bilioni nane (8) zimetumika kwa wanajeshi wa serikali na wakujitolea pamoja na mashahidi na majeruhi.

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuadhimisha mwaka wa pili tangu kutolewa kwa tangazo la ushindi dhidi ya magaidi wa Daesh iliyo fanyika siku za nyuma, kamati ya ustawi wa jamii chini ya kitengo cha Dini katika Ataba tukufu imetangaza kiwango cha pesa iliyo tumika kwa ajili ya wanajeshi wa serikali, wapiganaji wa kujitolea, mashahidi na majeruhi, tangu kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda hadi wakati wa kuandaa ripoti hii, karibu dinari za kiiraq bilioni nane (8) zimetumika, na bado tunaendelea kutoa misaada hadi sasa.

Kuhusu matumizi ya pesa hiyo; kamati imesema kua zilitumika chini ya utaratibu na mgawanyo ufuatao:

  • - Kusaidia wapiganaji kwenye uwanja wa vita, ikihusisha kugawa pesa za kujikimu, miwani ya usiku, nguo za kijeshi, chakula kibichi na kilicho pikwa, pamoja na vitu vingine.
  • - Kuwasiliana na familia za mashahidi na kutoa msaada wa kipesa kwa kila familia ya shahidi, ambazo hukabidhiwa kwa familia baada ya kuitembelea au kuiomba ifike kwenye kituo cha karibu yake au ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, au kwa maelekezo ya familia pale ambampo haijatembelewa.
  • - Kuwasiliana na majeruhi wa hashdi Shaábi na askari wa serikali pamoja na kuwatembelea katika nyumba zao au hospitalini, na kuwapa msaada wa pesa kwa ajili ya kuwasaidia kwenye matibabu yao.
  • - Kutoa zawadi za pesa kwa wapiganaji wa Hashdi Shaábi wasio kua na mishahara au wenye matatizo ya kibinaadamu.
  • - Kugharamia matibabu ya majeruhi au mwanafamilia kwa kulipa gharama za matibabu au kumpeleka kwenye hospitali ya rufaa Alkafeel.

Kumbuka kua lengo la program hii ni kusaidia wapiganaji wa kujitolea walio itikia wito wa Marjaa Dini mkuu wa kulinda Iraq na maeneo matukufu, pia ni sehemu ya kufanyia kazi maagizo ya Marjaa Dini mkuu ambaye amesisitiza na akahimiza kuwasaidia askari na Hashdi Shaábi kwa ajili ya kuwapa nguvu ya kuendelea kupambana, ukizingatia kua wapiganaji wa Hashdi Shaábi wanaupungufu mkubwa wa vifaa na mali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: