Kwa picha: ndani haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imesomwa dua ya kuliombea amani taifa la Iraq na raia wake.

Maoni katika picha
Wananchi wa Iraq hawaja acha kutembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kumtumikia, watumishi wa malalo hiyo takatifu wamezowea kuliombea dua taifa kila siku ya Jumanne na Alkhamisi ya kila wiki, huwa wanaliombea amani na utulivu pamoja na kuwarehemu mashahidi wa taifa hili.

Watumishi wa myweshaji wenye kiu Karbala (a.s), Adhuhuri ya Jumanne (3 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (12 Desemba 2019m) walifanya program ya kiibada, baada ya kusoma ziara na wimbo wa Ataba tukufu (Lahnul-Iba) na kumsalimia Abulfadhil Abbasi (a.s), walianza kuliombea dua taifa la Iraq, wakishirikiana na kundi kubwa la mazuwaru waliokua wamebeba bendera za Iraq pamoja na kuwarehemu mashahidi watukufu wa taifa hili).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: