Atabtu Abbasiyya inafanya hafla ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Aqilatu Twalibina bibi Zainabu (a.s).

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Aqilatu Twalibina bibi Zainabu Alkubra (a.s), Atabatu Abbasiyya kupitia kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kwa kushirikina na kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya jioni ya Jana Juma Nne (4 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (31 Desemba 2019m), imefanya hafla kubwa ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kushiriki kundi kubwa la mazuwaru.

Hafla imefunguliwa kwa Quráni, tukufu ukafuata ujumbe uliotolewa na Shekh Daakhil Nuri kutoka kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, akaeleza utukufu wa tukio hili kwa waumini pamoja na historia ya bibi Zainabu (a.s) na heshima aliyo kua nayo mbele ya kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), sambamba na kuelezea uchamungu wake na elimu aliyo chota katika nyumba ya Mtume, aidha akaeleza namna alivyo endeleza harakati ya Imamu Hussein (a.s) kupitia ulimi wake, hakika alikua balozi wa Imamu Hussein (a.s) aliendeleza harakati baada ya vita ya Twafu.

Halafu ukafuata wakati wa mashairi, akapanda kwenye mimbari mshairi Nizaar Habibi Hasanawi, halafu akapanda Farasi Asadi kasha akapanda Zainul-Abidina Saidi, wakasoma mashairi yaliyo onyesha mapenzi na utukufu wa Jabali wa subira bibi Zainabu (a.s).

Hafla ilihitimishwa kwa kusoma qaswida kuhusu tukio hilo adhim, hapo akapanda kwenye mimbari Hussein Akili na kuimba kaswida murua yenye maneno mazuri na sauti mutriba katika nyoyo za wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kufuatia sherehe za mazazi haya matukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: