Kutokana na maadhimisho ya (99) ya kuanzishwa kwake: kikosi cha Abbasi cha wapiganaji kimesisitiza kuendelea kusaidiana na jeshi katika kufikia malengo yake matukufu.

Maoni katika picha
Kutokana na maadhimisho ya miaka (99) tangu kuanzishwa jeshi shupavu la Iraq, kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji Liwaau/26 Hashdi-Shaábi kimetoa tamko, na ifuatayo ni nakala ya tamko hilo:

Katika wakati ambao uongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) unatoa salamu za pongezi kwa jeshi letu la Iraq, kutokana na kufikisha miaka tisini na tisa tangu kuanzishwa kwake, jeshi ambalo bado linaendelea kua ngome imara ya taifa na ngao madhubuti, pia tunatoa shukrani nyingi kwa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Sistani, kutokana na malezi yake ya ubaba kwa jeshi letu tukufu, hakika hajawaacha watoto wake bila kuwapa muongozo na maelekezo, amekua msaada mkubwa wakati wa shida.

Tunapokumbuka damu za wanaeshi zilizo mwagika wakati wa kulinda taifa na raia wake watukufu, hususan walio pata shahada kwenye vida dhidi ya Daesh, tunasisitiza kua kikosi hiki kimeshikamana na malengo ya kuanzishwa kwake sambamba na kushirikiana na jeshi hilo, ili kufanikisha malengo yake, hali kadhalika tumemuandaa mama na vijana wa Hashdi Sha,abi, ili waweze kutekeleza wajibu wao kulingana na changamoto tarajiwa.

Katika maadhimisho haya tunawakumbuka mashahidi wetu walio mwagilizia mti wa milele kwa damu zao takatifu, na wakajitolea kusimama pamoja na raia wao kwa nguvu zote hadi walipo pata ushindi dhidi ya adui.

Tunawatakia rehema za milele mashahidi wetu watukufu, na kupona haraka majeruhi wetu vipenzi, tunazishukuru sana familia zao kwa kusimama pamoja nao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: