Baada ya maandamano hali haitakua kama ilivyokua kabla yake: watawala watambue hilo.. haya yalisemwa na Marjaa Dini mkuu.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu alisema kua, kukimbia au kuchelewesha kurekebisha mambo ni kujidanganya, akasisitiza kua hali haitakua kama ilivyo kua kabla ya maandamano haya.

Aliyasema hayo kwenye kutuba ya swala ya Ijumaa (17 Rabiul-Awwal 1441h) sawa na (15/11/2019m) iliyo tolewa na Mheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Wananchi hawajatoka kwenda kwenye maandamano kudai islahi (mabadiliko) kwa namna hii hapo awali, wala hawajawahi kuandamana kwa muda mrefu kiasi hiki, pamoja na kupata mitihani mingi kwenye maandamano haya lakini bado wamesimama imara na wanaendelea kuongezeka siku baada ya siku, kutokana na watawala wa serikali kulifanya taifa kama mali yao, wanagawana utajiri wa taifa na kufumbia macho ufisadi, hadi wamelifikisha mahala pasipo vumilika, na imekua vigumu kwa mwananchi wa kawaida kupata mambo madogo ya msingi katika maisha, pamoja na utajiri mkubwa wa taifa hili. Kama watawala bado wanafikiri kua wanaweza kukwepa kufanya mabadliko ya kweli wajue wanajidanganya, baada ya maandamano haya haiwezekani hali ikawa kama ilivyo kua awali, wanatakiwa watambue hilo).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: