Kwa nyoyo zilizo jaa huzuni na majonzi, baada ya Adhuhuri ya Alkhamisi (13 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (9 Januari 2020m), watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wameomboleza kifo cha Swidiiqah Kubra Fatuma Zaharaa (a.s), na kumpa pole Imamu Hujjat bun Hassan (a.f), walisimama kwa mistari ndani ya haram ya mnyweshaji wenye kiu Karbala wakiwa wameshika bendera za huzuni.
Kisha wakatembea kuelekea katika malalo ya bwana wa mashahidi (a.s), wakapitia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu huku wakiimba na kupiga matam kwa huzuni kubwa kutokana na msiba huu mkubwa katika nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), walipo karibia kwenye haram ya Imamu Hussein (a.s), waliwakuta ndugu zao watumishi wa bwana wa mashahidi (a.s) wamesimama kuwapokea na kushirikiana nao kumpa pole mwenye msiba Imamu Abu Abdillahi Hussein (a.s), na wakafanya majlisi ya pamoja ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) na mazuwaru waliokuwepo ndani hapo wakashiriki kwenye majlisi hiyo.
Fahamu kua wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kila sehemu ya dunia wanaomboleza msiba huu wa kuondokewa na mbora wa wanawake wa ulimwenguni Fatuma Batuli (a.s).