Muhimu na hivi punde.. nakala ya tamko la Marjaa Dini mkuu kuhusu hali inayo shuhudiwa katika taifa la Iraq kwa sasa…

Maoni katika picha
Mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa ya leo (14 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (10 Januari 2020m) iliyo swaliwa ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) amesoma nakala ya tamko kutoka kwa Marjaa Dini kuu huko Najafu.

Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amesema: mabwana na mabibi nakusomeeni nakala iliyotufikia kutoka ofisi ya Mheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Hussein Sistani katika mji wa Najafu:

Kwa jina la mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

Wakati wa mitihani na shida kuna haja kubwa ya kusaidiana na kuungana, hilo haliwezi kupatikana ispokua pale kila mtu atakapokua tayali kusamehe baadhi ya maslahi yake binafsi na akatanguliza maslahi ya umma.

Hakika kuamiliana kwa pande tofauti zenye nguvu na wafuasi, na kila moja ikitaka kulazimisha maoni yake kwa kundi lingine, kutapelekea kukuza tatizo na kushindwa kupata muwafaka, inawezekana makundi yote yakapata hasara, tena hasara kubwa ya taifa zima na watu wote, hadi wale wasiokua na mchango katika vita ya ndani na nje inayo endelea, wala hawajihusishi na jambo lolote kuhusu amani ya taifa lao na utulivu, kwa kua na maisha bora kwao na kwa watoto wao.

Yaliyotokea siku chache zilizo pita, shambulizi hatari na uvunjifu wa heshima ya taifa la Iraq, na udhaifu wa utawala katika kulinda taifa na raia wake, shambulio hilo na uvunjifu wa heshima, ni sehemu ya matatizo yanayo endelea, kila mtu anatakiwa atafakari hali itakuwa namna gani kama mambo haya yasipoisha, kila mtu akishikilia msimamo wake na akakataa kulegeza msimamo, bila shaka jambo hilo litasababisha matatizo kila sehemu, kwenye vyombo vya usalama, wanasiasa, uchumi na katika jamii, litatoa nafasi kwa watu wengine kuingilia mambo ya taifa letu na kutumia fursa hiyo kufanikisha mambo yao.

Kila mtu akiwa mzalendo na akiwajibika kwa taifa lake, akitafuta dawa ya matatizo tunayo pitia kwa sasa, akakubali kufanya mabadiliko yanayo takiwa chini ya utaratibu uliopangwa na kuzungumzwa mara nyingi, tutatoka salama kwenye matatizo haya kama tunataka kuyamaliza kwa njia inayo kubalika, baada ya kujitolea sana wananchi wa taifa hili katika maeneo mbalimbali.

Inatosha, wananchi wamehangaika kwa muda mrefu katika vita na mitihani ya kila aina kwa miongo mingi, chini ya tawala zilizo pita hadi utawala wa sasa, kila mtu ahisi kuwajibika kwa taifa lake wala msipoteze fursa ya kutengeneza mustakbali bora wa taifa hili, kila mtu anamatarajio makubwa ambayo hayajafikiwa hadi leo, taifa la Iraq linatakiwa kujitawala na kua na maamuzi yake bila kuingiliwa na mataifa ya kigeni, maamuzi yake yatokane na matashi ya wananchi, kuwe na utawala bora unaomjali kila raia bila kuangalia kabila yake wala dini yake, na kuhakikisha wananchi wanakua na maisha bora yenye amani na utulivu, je jambo hili ni gumu kwa taifa hili ambalo linamiliki watu wenye akili sana na uwezo mkubwa?! Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atuwezeshe kupita katika njia hii hakika yeye ni mwingi wa rehema mwenye kurehemu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: