Marjaa Dini mkuu amesisitiza kua taifa la Iraq linatakiwa lijitawale wala lisiwape nafasi wageni katika maamuzi yake.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesisitiza kua taifa la Iraq linatakiwa lijitawale wala lisitoe nafasi kwa watu wa nje kuingilia mambo yake ya ndani, maamuzi yake yanatakiwa yatokane na matakwa ya wananchi, kuwe na utawala bora unao watumikia raia wote bila kuangalia tofauti zao za kikabila au kidini, akasema kua matatizo waliyo pata wananchi ya vita na mitihani mbalimbali kwa muda mrefu yanatosha, chini ya tawala zilizo tangulia hadi utawala huu.

Ameyasema hayo kwenye khutuba ya Ijumaa leo (14 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (10 Januari 2020m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), iliyosomwa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Inatosha, wananchi wamehangaika kwa muda mrefu katika vita na mitihani ya kila aina kwa miongo mingi, chini ya tawala zilizo pita hadi utawala wa sasa, kila mtu ahisi kuwajibika kwa taifa lake wala msipoteze fursa ya kutengeneza mustakbali bora wa taifa hili, kila mtu anamatarajio makubwa ambayo hayajafikiwa hadi leo, taifa la Iraq linatakiwa kujitawala liwe na maamuzi yake bila kuingiliwa na mataifa ya kigeni, maamuzi yake yatokane na matakwa ya wananchi, kuwe na utawala bora unaomjali kila raia bila kuangalia kabila yake wala dini yake, na kuhakikisha wananchi wanakua na maisha bora yenye amani na utulivu, je jambo hili ni gumu kwa taifa hili ambalo linawatu wenye akili sana na uwezo mkubwa)?!
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: