Kwa mazuwaru: Haya ndio yaliyofanywa na Masayyid katika kuomboleza kifo cha bibi yao Zaharaa (a.s).

Maoni katika picha
Kuna mambo wamezowea kuyafanya masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuomboleza kifo cha bibi yao Fatuma Zaharaa (a.s), miongoni mwa mambo hayo ambayo hufanywa kila mwaka katika msimu huu ni kugawa chai kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Shughuli hiyo huanza kufanywa wakati wa kuomboleza kifo cha Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya pili ambapo tupo katika siku hizo, zinazo itwa (msimu wa pili wa huzuni za Fatwimiyya), utawakuta Masayyid wanashindana kufanya huduma hiyo ndogo yenye malengo makubwa.

Utawakuta mazuwaru wanasimama mistari kuchukua chai wanayo pewa na mikono ya ma-alawi jirani na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na udogo wa jambo hili lakini hupata mwitikio mkubwa, kwa sababu linafanyika jirani na mahala patakatifu, na huduma inatolewa na Masayyid ambao ni wahudumu wa Ataba tukufu pamoja na watu wa kujitolea kutoka nje ya Ataba, baada ya watu kufanya ziara na kuomba dua huja kunywa chai hiyo ya aina yake.

Kumbuka kua Masayyid ambao ni watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) husimamia kazi hiyo chini ya umoja wao ujulikanao kama (Idara ya Masayyid watumishi), idara hiyo inamajukumu mengi, na huongezeka majukumu yao katika msimu wa ziara zinazo hudhuriwa na watu wengi pamoja na siku za kuomboleza vifo vya maimamu wa Ahlulbait (a.s), ikiwemo kumbukumbu ya kifo cha bibi Zaharaa (a.s), wanautaratibu maalum wa kuomboleza matukio hayo kama vile kufanya majlis na kushiriki katika mawakibu za waombolezaji na watoa huduma, utawakuta ndani na nje ya haram tukufu wakiwa wamevaa nguo maalum zinazo mpa zaairu utulivu wa nafsi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: