yaliyo semwa na Marjaa Dini mkuu: Kama tunakaribisha msaada wowote haimaanishi kuacha utambulisho na uhuru wetu.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesisitiza mara nyingi kupitia khutuba za Ijumaa, kuhusu umuhimu wa utambulisho na uhuru wa Iraq, na kutolifanya taifa la Iraq kua uwanja wa vita ya kieneo na kimataifa na kujiepusha na fikra mbaya walizo nazo baadhi ya watu.

Tujikumbushe baadhi ya yaliyosemwa na Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya Ijumaa miaka ya nyuma, mwezi (21 Jamadal-Uula 1436h) sawa na (13 Machi 2015m), iliyo swaliwa ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi:

(Kama tunakaribisha msaada wowote kutoka kwa ndugu zetu na marafiki zetu kwa ajili ya kupigana na magaidi na tunawashukuru kwa misaada hiyo, hilo halimaanishi kuacha utambulisho na uhuru wetu, hatutakiwi kuwa sehemu ya kuunga mkono fikra potofu za baadhi ya viongozi, hakika tunaandika historia yetu kwa damu za mashahidi wetu na majeruhi wetu katika vita tunayo pigana leo dhidi ya magaidi, damu ya tabaka zote za wananchi wa Iraq imechanganyika).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: