Kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinashiriki katika maonyesho ya tisa ya katiba na sheria yanayo simamiwa na mahakama kuu ya mji wa Basra, ambayo hushiriki taasisi mbalimbali za uchapaji na usambazaji.
Makamo mkuu wa kituo cha turathi za Basra Ustadh Yasini Yusufu ameongea na mtandao wa Alkafeel kua: “Kituo cha turathi kinashiriki kwa mara ya tatu mfululizo katika maonyesho ya vitabu vya mahakama kuu ya Basra, kwa mwaliko wa mawakili wa kiiraq katika mji huo, nacho kimeonyesha machapisho ya (kimazingiri, kijamaa, kidini na kifikra), pamoja na nakala kale na nyaraka zingine”.
Akaongeza kua: “Muitikio wa watu wa Basra katika kuangalia vitabu hivyo ni mzuri, pamoja na kuwepo kwa vitabu vya kielektronik bado kuna watu wanapenda kusoma vitabu halisi”.
Ushiriki wa maonyesho haya umekua na matokea mazuri, kila mtu amesifu ushiri wa kitengo chetu na ubora wa machapisho yake, pamoja na kushukuru harakati zote zinazo fanywa na kituo, wanathamini nafasi ya kituo katika kuhuisha turathi za Basra.