Muhimu.. kwa video: Sayyid Ahmadi Swafi na jopo la madaktari wameongea na waandishi wa habari kuhusu upasuaji aliofanyiwa Marjaa Dini mkuu

Maoni katika picha
Mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na jopo la madaktari walio mfanyia upasuaji Marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani, wameongea na waandishi wa habari kuhusu upasuaji huo ulio fanywa leo katika hospitali ya rufaa Alkafeel ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Sayyid Ahmadi Swafi amesema kua: “Tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa neema aliyo tupa, Mheshimiwa Sayyid jana alipata maumivu kwenye mguu wake, yaliyo tokana na kuvunjika mfupa wa paja la kushoto”.

Akaongeza kua: “Allah ashukuriwe, madaktari walikusanyika na kuangalia hali yake sambamba na kumfanyia vipimo vya lazima kwa maandalizi ya kumfanyia upasuaji”.

Akabainisha kua: “Tunamshukuru Allah kazi ya upasuaji imekamilika ndani ya nusu saa chini ya jopo la madaktari mahiri, wametuambia kua hali ya Mheshimiwa ni nzuri, baada ya siku chache atarudi katika hali ya kawaida”.

Akaongeza kua: “Jopo la madaktari waliomfanyia upasuaji liliongozwa na dokta Adnani Karbalai mbobezi wa upasuaji, pamoja na dokta Ihsani Muhammad Ali Faraji, dokta Ahmadi Ni’matu Twaaiy, dokta Bariri Muhammad Ali Asadiy na dokta Haitham Mahmudu Asadiy”.

Akasisitiza kua: “Upasuaji umefanywa baada ya uchunguzi wa kina, tunamshukuru Mwenyezi Mungu Sayyid anaendelea vizuri”.

Naye Dokta Ihsani Faraji akabainisha kua: “Mwenyezi Mungu mtukufu ametuwezesha mimi na wenzangu chini ya uongozi wa Dokta Adnani kufanya upasuaji wa kurekebisha mfupa wa paja la kushoto la Mheshimiwa Sayyid”.

Akabainisha kua: “Kutokana na ukubwa wa umri wa Mheshimiwa Sayyid hupelekea kupata tatizo la mifupa, mfupa wake umevunjika sehemu ambayo hupona haraka, tumemfanyia upasuaji mdogo wa kurekebisha mfupa, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu baada ya matibabu haya mfupa utakua imara, na kesho tunaweza kuanza kumsimamisha kwa miguu yake”.

Akasisitiza kua: Upasuaji ulifanyika kwa kuondoa hisia sehemu yenye tatizo, wakati wote wa upasuaji Mheshimiwa alikua analiombea dua taifa la Iraq na raia wake, na sasa hivi anahisi kupona baada ya upasuaji, kwa ujumla kazi ilikua nzuri tunamshukuru Mwenyezi Mungu, afya yake itaimarika Insha-Allah”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: